Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Kor 6

6
1 # 2 Kor 1:24; 5:20 Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. 2#Isa 49:8; Lk 4:19,21(Kwa maana asema,
Wakati uliokubalika nalikusikia,
Siku ya wokovu nalikusaidia;
tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.) 3Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; 4#2 Kor 4:2bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida; 5#Mdo 16:23; 2 Kor 11:23-27katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; 6#1 Tim 4:12katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki; 7#1 Kor 2:4katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; 8kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; 9#2 Kor 4:10; Zab 118:18kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; 10#Flp 4:12,13kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
11 # Zab 119:32 Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa. 12Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu. 13#1 Kor 4:14Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo.
Hekalu la Mungu Aliye Hai
14 # Efe 5:11 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?#6:15Beliari maana yake ni, Ufisadi. Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16#Law 26:12; Eze 37:27; 1 Kor 3:16; 6:19; Eze 37:27Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17#Isa 52:11; Yer 51:45; Eze 20:34,41; Ufu 18:4Kwa hiyo,
Tokeni kati yao,
Mkatengwe nao, asema Bwana,
Msiguse kitu kilicho kichafu,
Nami nitawakaribisha.
18 # 2 Sam 7:8,14; 1 Nya 17:13; Isa 43:6; Yer 31:9; 32:38; Hos 1:10; Amo 4:13 Nitakuwa Baba kwenu,
Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,
asema Bwana Mwenyezi.

Iliyochaguliwa sasa

2 Kor 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha