Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kinazungumzia Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu, ili awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo yalitarajiwa kutukia karibuni. Ijapokuwa kitabu kimechukua jina la mwandishi, “Ufunuo wa Yohana,” ukweli ni kwamba hakimzungumzii Yohana wala hakimfunui yeye, bali kinamzungumzia na kumfunua Yesu Kristo. Yesu ndiye Mwana-Kondoo ambaye ameleta ukombozi. Yeye ndiye atakayehukumu na kushinda kabisa uovu, ili Ufalme wa milele ulio bora kabisa uthibitishwe.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Kusudi
Kuwahimiza waumini kukataana na shinikizo la kumwabudu mfalme, na kusimama imara katika majaribu mpaka kifo.
Mahali
Kisiwa cha Patmo, karibu na pwani ya Uyunani (Ugiriki).
Tarehe
Kama 95 B.K.
Wahusika Wakuu
Yohana na Yesu.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinamwonyesha Yesu kuwa ndiye Mwana-Kondoo aliyechinjwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, na akileta utawala wa haki milele na milele.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinatumia lugha ya kiufunuo, yaani matumizi ya mifano, na majina ya kufananisha, ndoto, maono, matumizi makubwa ya tarakimu, na pia viumbe vya mbinguni na vya dunia vya kutisha. Kinaonyesha mambo yale Yohana aliyoyaona, yaani maono ya Yesu Kristo akiwa katikati ya kile kinara cha taa. Nayo mambo yaliyopo ina maana zile barua saba kwa makanisa saba katika Asia Ndogo. Nayo mambo ambayo hayana budi kutukia baada ya hayo inaweza kumaanisha matukio baada ya kunyakuliwa kwa kanisa.
Mgawanyo
Mwanzo wa maono kuhusu Yesu Kristo (1:1-20)
Barua saba kwa Makanisa saba (2:1–3:22)
Maono kuhusu Mungu na Mwana-Kondoo (4:1–5:14)
Lakiri saba za hukumu (6:1–8:5)
Tarumbeta saba za hukumu (8:6–11:19)
Maono kuhusu vita ya duniani na mbinguni (12:1–14:20)
Mabakuli saba ya hukumu (15:1–16:21)
Hukumu juu ya Kahaba Babeli (17:1–19:21)
Mwisho wa nyakati, na wakati ujao (20:1–22:21).

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha