Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mika Utangulizi

Utangulizi
Jina Mika maana yake ni “Ni nani aliye kama Bwana.” Mika aliishi wakati mmoja na Isaya na Hosea. Aliona Waashuru wakiendelea kustawi wakati Israeli ilikuwa ikididimia hadi ikawa jimbo la Ashuru baada ya kuanguka kwa Israeli mwaka wa 722 K.K. Yuda mara kwa mara ilipata vitisho kutoka kwa wafalme wa Ashuru waliofanikiwa. Mika alionya juu ya hukumu ya Mungu dhidi ya falme zote mbili za Yuda na Israeli. Alitabiri kuwa miji hiyo ingeangamizwa kwa sababu ya watawala wake waovu, manabii wa uongo, makuhani waovu, wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu, na mahakimu waliopokea rushwa na kwa hivyo walishindwa kuonyesha hali ya uchaji na hofu ya Mungu katika wajibu wao.
Kinyume na hayo, Mika alitoa ahadi ya kufanywa upya kwa Sayuni na utawala wa amani kwa wale waliomwamini na kumtumaini Mungu. Alitabiri kwamba Sayuni iliyofanywa upya itakuwa kitovu cha utawala wa ulimwengu wote, mahali ambapo amani halisi na haki vitatawala. “Mtawala katika Israeli” ambaye angelizaliwa Bethlehemu, angesimamisha utawala ambao ungedumu milele.
Mwandishi
Mika, mwenyeji wa Moreshethi, karibu na Gathi.
Kusudi
Kuwaonya watu wa Mungu kuhusu hukumu iliyokuwa inakaribia, na kuwasamehe wote waliotubu.
Mahali
Samaria na Yerusalemu.
Tarehe
Kati ya 742–687 K.K.
Wahusika Wakuu
Watu wa Samaria na Yerusalemu.
Wazo Kuu
Kuwaonya watu juu ya dhambi za udhalimu, uchoyo, ufisadi na ibada za sanamu, vitu ambavyo vingesababisha hukumu iwapo watu wasingetubu na kuacha njia zao mbaya.
Mambo Muhimu
Huu ni mfano mzuri wa ushairi wa Kiebrania. Ziko sehemu tatu, kila moja ikianza na “Sikia” au “Sikiliza” (1:2; 3:1; 6:1) na kufunga na ahadi.
Mgawanyo
Hukumu dhidi ya Samaria na Yerusalemu (1:1-16)
Uonevu wa viongozi (2:1–3:12)
Urejesho wa Mungu (4:1–5:15)
Hukumu na huruma (6:1–7:20).

Iliyochaguliwa sasa

Mika Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha