Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yuda Utangulizi

Utangulizi
Mwandishi wa waraka huu ni Yuda, aliyekuwa nduguye Yakobo, yule aliyekuwa msimamizi wa baraza la Yerusalemu, na mwandishi wa waraka wa Yakobo. Alikuwa ndugu wa Yesu kwa kuzaliwa na Maria (Marko 6:3).
Muktadha wa waraka huu na yale yaliyomo kwenye waraka wa 2 Petro yanaashiria kuwa Yuda alikuwa amehamasishwa na ujumbe wa Petro. Yuda anaonyesha kuwa alikusudia kuandika kuhusu wokovu, lakini akabadili nasaha zake ili kukemea mtazamo wa watu fulani wenye tabia mbaya, waliokuwa wakizunguka miongoni mwa waumini wakipotosha neema ya Mungu.
Mwandishi
Yuda, ndugu yake Yesu.
Kusudi
Kukumbusha kanisa umuhimu wa kuitetea imani, na kulionya juu ya watu waovu wanaozunguka miongoni mwao wakipotosha imani.
Mahali
Hapajulikani.
Tarehe
Kama 65 B.K.
Wahusika Wakuu
Yuda, Yakobo, na Yesu.
Wazo Kuu
Yuda anasisitiza umuhimu wa kuitetea imani. Wapotovu na wazushi ni lazima waonyeshwe wazi kwamba sio wa kweli. Yuda anaonya kwamba hukumu ya Mungu itawafikia wale waliopotoka katika imani, kama vile ilivyowafikia Kaini, Kora, na Balaamu.
Mambo Muhimu
Kuweka wazi walimu wa uongo na kuwakemea vikali. Anamalizia ujumbe wake kwa kuonyesha wazi kwamba Mungu anaweza kumlinda muumini, ili aweze kuishi maisha yaliyonyooka, na hatimaye kufika mbele ya Mungu bila lawama wala mawaa.
Mgawanyo
Utangulizi (1-4)
Maonyo dhidi ya uongo (5-16)
Adibisho na hitimisho (17-25).

Iliyochaguliwa sasa

Yuda Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha