Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya Utangulizi

Utangulizi
Jina Isaya maana yake ni “Bwana anaokoa.” Kufuatana na mapokeo, Isaya alitoa unabii wakati mmoja na Amosi, Hosea na Mika. Isaya alianza huduma yake mwaka wa 740 K.K. Isaya alikuwa ameoa, na akapata watoto wawili, Shear-Yashubu na Maher-Shalal-Hash-Bazi. Yamkini, Isaya alitumia wakati wake mwingi huko Yerusalemu wakati wa Mfalme Hezekia. Kufuatana na historia ya Kiyahudi, Isaya aliuawa kwa kupasuliwa vipande viwili chini ya utawala wa Manase, yule mwana mwovu wa Mfalme Hezekia, aliyetawala tangu 696–642 K.K.
Mwandishi
Isaya mwana wa Amozi.
Kusudi
Isaya anatoa wito kwa taifa la Yuda kumrudia Mungu, na pia anawatangazia wokovu wa Mungu kupitia kwa Masiya.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
700–680 K.K.
Wahusika Wakuu
Isaya, wanawe wawili Shear-Yashubu na Maher-Shalal-Hash-Bazi, Mfalme Hezekia.
Wazo Kuu
Kuufanya ujumbe wa Mungu uwe wazi kwa Israeli, ili kuwaonya kuhusu hukumu ikiwa wataendelea kudumu katika dhambi. Pia kudhihirisha jinsi Mungu atakavyoshughulika nao katika kukamilisha kuwarejesha upya chini ya Masiya wao milele.
Mambo Muhimu
Mungu atamtuma Masiya ili kuokoa watu wake; atakuja kama Mwokozi na Bwana pekee, lakini atatenda kama mtumishi. Atakufa ili kuziondoa dhambi. Mungu anaahidi kutuma faraja, ukombozi na urejesho katika ufalme wake ujao. Masiya atatawala juu ya wafuasi wake wakati huo. Tumaini ni hakika kwa sababu Kristo yuaja.
Mgawanyo
Hukumu na matumaini ya matengenezo (1:1–6:13)
Matumaini kwa Ashuru au Mungu (7:1–12:6)
Unabii kuhusu mataifa (13:1–23:18)
Hukumu ya Israeli na ukombozi (24:1–27:13)
Maonyo, na Sayuni yatengenezwa (28:1–35:10)
Mfalme Hezekia awazuia Waashuru (36:1–39:8)
Ahadi za ukombozi wa Mungu (40:1–56:8)
Ufalme wa mwisho unasimamishwa (56:9–66:24).

Iliyochaguliwa sasa

Isaya Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha