Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wathesalonike Utangulizi

Utangulizi
Waraka huu uliandikwa miezi michache tu baada ya ule wa kwanza. Baadhi ya watu walikuwa wamemwelewa vibaya Paulo, au waraka mwingine wa bandia uliosemekana kuwa ulitoka kwa Paulo ulikuwa umewafadhaisha Wathesalonike kuhusu kurudi kwa Yesu. Paulo aliandika waraka huu ili kuwakumbusha yale aliyokuwa ametangulia kuwafundisha, akiwahakikishia waumini kuwa Kristo atarudi kuwafariji waliomwamini na kuwaadhibu wale waliokuwa wakiwatesa. Aliwaambia kwamba siku ya Bwana, yaani siku ya hukumu, haitawafikia mara moja, bali itatanguliwa na matukio mbalimbali. Wakifahamu kuwa hakika Kristo atarudi, basi iliwapasa waumini kuishi maisha matakatifu yasiyo na lawama.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuondoa mkanganyiko kuhusu kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili.
Mahali
Korintho.
Tarehe
Kati ya 51–52 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Silvano, na Timotheo.
Wazo Kuu
Kuwafariji Wathesalonike kwa ajili ya mateso, na kuwahimiza waishi maisha ya kumtukuza Mungu.
Mambo Muhimu
Kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili, na kuwaonya waumini wasiache kufanya kazi.
Mgawanyo
Faraja kutokana na kurudi kwa Kristo (1:1-12)
Matukio kabla ya kuja kwa siku ya Bwana (2:1-12)
Maagizo zaidi na maonyo (2:13–3:5)
Mausia ya Kikristo, na kuwatakia heri (3:6-18).

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha