Leseplan-informasjon

BibleProject | Kumwamini Mungu katika MatesoPrøve

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

Dag 6 av 6

Kitabu cha Ayubu kinamalizikia Mungu akirejesha kila kitu ambacho Ayubu alipoteza. Hii inatufundisha nini? Kwanza, hebu tukumbuke kwamba simulizi hii tayari imetuonyesha kwamba haki ya Mungu ni kuu kuliko mtazamo kuwa wenye haki hutunzwa nao waovu huadhibiwa. Japo ni kweli kwamba Mungu huwazawadia wanaomcha (Waebrania 11:6) na kuwa huadhibu uovu kwa haki (Isaya 13:11), sifa hizi za Mungu hazifanyi kazi kila wakati katika njia ambazo tunatarajia. Hivyo Mungu kurejesha afya na mali ya Ayubu haikuwa kwa sababu ya utakatifu wa Ayubu, na pia Ayubu kupoteza mali yake haikuwa adhabu kutoka kwa Mungu. Hitimisho la kitabu linaonyesha kuwa haijalishi yanayotendeka maishani mwetu, mema au mabaya, tunaweza kumtegemea Mungu kuwa mkarimu na tunaweza kutegemea nguvu zake za kurejesha. Tunapomalizia siku ya mwisho kwenye mwongozo wa kusoma, hebu tupitie tulichojifunza. Tazama video yetu ya Muhtasari kuhusu kitabu cha Ayubu ili uangalie mpangilio wake na mtiririko wa matukio. TAFAKARI: 1) Je, unaweza kuandaa muhtasari wako mwenyewe kuhusu ujumbe wa video uliyotazama? 2) Je, mwongozo huu wa kusoma umekusaidia vipi kuelewa au kuchambua kitabu cha Ayubu? 3)Je, unaweza kushiriki mwongozo huu na nani siku ya leo?

Skriften

Dag 5

Om denne planen

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

Je, tunawezaje kumwamini Mungu hata pale tunapoteseka bila kustahili? Jiunge nasi katika muongozo huu wa wa siku zita unaotazama simulizi ya Ayubu na ufahamu jinsi kuamini hekima ya Mungu kunaonekaje hata katika vipindi ...

More

YouVersion bruker informasjonskapsler for å tilpasse opplevelsen din. Ved å bruke nettstedet vårt godtar du vår bruk av informasjonskapsler, som beskrevet i vår Personvernerklæring