Leseplan-informasjon

BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 4 av 32

Sura ya 3: Ya Thamani kuliko Vito Katika sura hii baba anamzungumzia tena mwanawe mara mbili, na lipo shairi kumhusu Binti Hekima. Baba Anamzungumzia Mwanawe Mara ya Tatu Mstari wa 1-12: Hotuba hii ni nzito na inajumuisha vifungu maarufu. Baba anaacha sisitizo la hapo awali kuhusu kuenea kwa maovu na anamhimiza mwanawe kushughulikia tabia yake mwenyewe. Chunguza matumizi ya maneno na jinsi baba anarudia neno "wewe/yako" kuonyesha matendo binafsi ya imani na matokeo yake. Mpe Mungu kilicho bora zaidi ("Mazao yako ya kwanza") na utakuwa na utele ("maghala yako yatajaa na kufurika") Mistari miwili ya mwisho katika sehemu hii (11-12) ni tofauti kwa kuwa haiangazii manufaa ya kumheshimu Mungu. Badala yake, baba anamhimiza mwanawe kukubali nidhamu ya Mungu. Usiwe na uchungu mambo yakiwa magumu, anasema, ila amini kuwa Mungu huwakosoa Anaowapenda—kama baba kumwadhibu mwanawe. Binti Hekima Anazungumza Mara ya Pili Mstari wa 13-20: Hili ni shairi nzuri kuhusu hekima, na linamtumia tena mwanamke kama mhusika. "Ni wa thamani kuliko marijani; mwandishi anasema, "hakuna unachotamani kinachoweza kulinganishwa naye." Mshairi anamfafanua Binti Hekima kama mahali pa tulivu, mahali pa kupumzika na kiini cha amani—chenye uwezo. Analinganishwa na "mti wa uzima" kwenye kitabu cha Mwanzo 2:9, na katika mstari wa 19-20 tunaambiwa kuwa Mungu mwenyewe alitumia hekima kuumba ulimwengu: "Kwa hekima Mungu Aliiweka misingi ya dunia." Hekima ya Mungu ina uwezo mkuu katika ulimwengu huu na tunaweza kuipata! Baba Anazungumza na Mwanawe Mara ya Nne Mstari wa 21-35: Sura hii inaishia na hotuba nyingine kutoka kwa baba, akisisitiza tena kuwa njia ya hekima ni njia ya amani. Ukiwa mwenye hekima, utalala vyema, utaishi bila hofu na utajiepusha na mitego ambayo watu wengine huingia kwa urahisi. Baba anatoa ushauri kuhusu uhusiano unaolenga kuleta amani: lipa unachodaiwa, usiwadhuru watu, usiwashtaki watu bila ushahidi, na usitamani mali ambayo watu wanapata kupitia ukatili.
Dag 3Dag 5

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu ...

More

YouVersion bruker informasjonskapsler for å tilpasse opplevelsen din. Ved å bruke nettstedet vårt godtar du vår bruk av informasjonskapsler, som beskrevet i vår Personvernerklæring