Leseplan-informasjon

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaPrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Dag 7 av 20

Baada ya kusoma mafundisho ya Yesu kuhusu Ufalme wake unaoenda kinyume na matarajio, huenda tukaanza kuhoji kuhusu ukuu wa mfalme aliyefundisha kuwa, "mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili”. Lakini neema ya Yesu si udhaifu. Tunapoendelea kusoma, tunaona kwamba Mfalme Yesu ana uwezo wa kuwafufua hata wafu. Watu wengi wanaomwona na kumsikia Yesu akitenda miujiza hii yote ya kushangaza wanafahamu kuwa ni kupitia nguvu ya Mungu. Lakini Yohana Mbatizaji hawezi kuona wala kusikia yote yanayoendelea akiwa gerezani. Yohana anaanza kuwa na tashwishi ikiwa kweli Yesu ndiye Masihi. Yesu anatuma ujumbe kwa Yohana kwa kumnukuu tena nabii Isaya: “maskini wanahubiriwa habari njema.” Yohana anajua kuwa neno hili linamrejelea Masihi anayetarajiwa. Lakini pia anafahamu kuwa vifungu vinavyofuata kwenye maandiko ya Isaya vinatabiri kuwa Masihi atanena “uhuru kwa waliofungwa,” iweje Yohana bado ni mfungwa? Je, Yesu alimsahau? Yesu anaona dhiki ya Yohana na anatoa ahadi, “amebarikiwa asiyechukizwa nami.” Lakini wengi wanagoma kuipokea baraka hii na wanaghadhabishwa na Yesu, hasa viongozi wa dini. Hawaelewi kwa nini Yesu ni mkarimu kwa watu wa nje ambao maisha yao ni ya kuchukiza. Lakini Yesu anajua jinsi ya kuwarekebisha wanapoletwa kwake. Kwa mfano, Luka anasimulia kuwa mwanamke mmoja kwenye karamu anaponyenyekea na kuipangusa miguu ya Yesu huku akimdondoshea machozi ya shukrani, Yesu anatakasa maisha yake yote kupitia msamaha wake. Na yuko tayari pia kutusamehe tunapomwendea. Huu ndio Ufalme unaoenda kinyume na matarajio. Huenda tunatarajia kuwa makosa yetu yatatutenganisha na mfalme, ila Yesu sio kama wafalme wengine. Ni mwenye neema na fadhili na anaingilika––hata kifo na kuta za gereza haziwezi kuwatenganisha watu wake na upendo wake. Soma, Tafakari, kisha Ujibu: •Jaribu kupata picha ungeshuhudia Yesu alipowafufua yule msichana na mvulana. Je, ungehisi vipi? Je, ungefanya nini? •Je, unahisi umesahaulika au hujahesabika katika kupokea baraka za Mungu? Yesu anahakikishia umati kuwa anatekeleza kazi yake na anawabariki wasiochukizwa wanapokosa kuona baraka zake. Je, unachukulia vipi hakikisho hili? •Mwanamke aliyepaka mafuta miguu ya Yesu hakuona haya kuonyesha upendo wake kwake. Je, unamjua mtu yeyote kama huyo? Je, mtu huyo huonyesha vipi upendo wake kwa Yesu? •Upendo wetu kwa Yesu unalingana na jinsi tunavyoelewa ukuu wa msamaha wake kwetu. Je, umemwomba Yesu akusamehe dhambi zako zote? Ikiwa umefanya hivyo, tafakari kuhusu msamaha wa Yesu kwako––waza kwa undani. Je, unaweza kuonyesha vipi upendo wako kwa Yesu leo? •Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba ombi la unyoofu kutoka moyoni mwako.
Dag 6Dag 8

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video z...

More

YouVersion bruker informasjonskapsler for å tilpasse opplevelsen din. Ved å bruke nettstedet vårt godtar du vår bruk av informasjonskapsler, som beskrevet i vår Personvernerklæring