YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 92

92
Wimbo wa kumsifu Mungu
(Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato)
1Ni vema kukushukuru, ee Mwenyezi-Mungu,
kuliimbia sifa jina lako, ee Mungu Mkuu.
2Ni vema kutangaza fadhili zako asubuhi,
na uaminifu wako nyakati za usiku,
3kwa muziki wa zeze na kinubi,
kwa sauti tamu ya zeze.
4Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha;
nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda.
5Matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, ni makuu mno!
Mawazo yako ni mazito mno!
6Mtu mpumbavu hawezi kufahamu,
wala mjinga hajui jambo hili:
7Kwamba waovu waweza kustawi kama nyasi,
watenda maovu wote waweza kufanikiwa,
lakini mwisho wao ni kuangamia milele,
8bali wewe, ee Mwenyezi-Mungu, u mkuu milele.
9Hao maadui zako, ee Mwenyezi-Mungu,
naam, hao maadui zako, hakika wataangamia;
wote watendao maovu, watatawanyika!
10Wewe umenipa nguvu kama nyati;
umenimiminia mafuta ya kuburudisha.
11Kwa macho nimeona maadui zangu wameshindwa;
nimesikia kilio chao watendao maovu.
12Waadilifu hustawi kama mitende;
hukua kama mierezi ya Lebanoni!
13Kama miti iliyopandwa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu,
hustawi katika nyua za Mungu wetu;
14huendelea kuzaa matunda hata uzeeni;
daima wamejaa utomvu na wabichi;
15wapate kutangaza kwamba Mwenyezi-Mungu ni mnyofu,
Mwamba wangu, kwake hamna upotovu.

Currently Selected:

Zaburi 92: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy