YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 77

77
Faraja wakati wa shida
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu)
1Namlilia Mungu kwa sauti,
kwa sauti namlilia Mungu anisikie.
2Wakati wa taabu namwomba Bwana;
namnyoshea mikono yangu usiku bila kuchoka,
lakini sipati faraja yoyote kwa mtu.
3Ninamfikiria Mungu na kusononeka;
ninatafakari na kufa moyo.
4Wanizuia hata kupata lepe la usingizi,
nina mahangaiko hata kusema siwezi.
5Nafikiria siku za zamani;
nakumbuka miaka ya hapo kale.
6Usiku nawaza na kuwazua moyoni;
natafakari na kujiuliza rohoni:
7“Je, Bwana ametuacha kabisa?
Je, hatatuonesha tena hisani yake?
8Je fadhili zake zimekoma kabisa?
Je, hatatimiza tena ahadi zake?
9Je, Mungu amesahau kuwa na huruma?
Je, hasira yake imeuondoa upole wake?”
10Kisha nikasema, “Kinachonichoma zaidi ni kwamba,
Mungu Mkuu hatendi tena kitu kwa ajili yetu!”
11Nitayakumbuka matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu,
naam, nitayafikiria maajabu yako ya hapo kale.
12Nitatafakari juu ya kazi zako,
na kuwaza juu ya matendo yako makuu.
13Kila ufanyacho ee Mungu, ni kitakatifu.
Ni mungu gani aliye mkuu kama Mungu wetu?
14Wewe ni Mungu unayetenda maajabu;
wewe umeyaonesha mataifa uwezo wako.
15Kwa mkono wako wa nguvu uliwakomboa watu wako;
uliwakomboa wazawa wa Yakobo na Yosefu.
16Maji yalipokuona, ee Mungu,
maji yalipokuona, yaliogopa mno;
naam, bahari ilitetemeka hata vilindini.
17Mawingu yalichuruzika maji,
ngurumo zikavuma angani,
mishale ya umeme ikaangaza kila upande.
18Kishindo cha ngurumo yako kilitokea katika kimbunga,
umeme wako ukauangaza ulimwengu;
dunia ikatikisika na kutetemeka.
19Wewe uliweka njia yako juu ya bahari;
ulitembea juu ya maji yale mengi,
lakini nyayo zako hazikuonekana.
20Uliwaongoza watu wako kama kondoo,
chini ya uongozi wa Mose na Aroni.

Currently Selected:

Zaburi 77: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy