YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 74

74
Ombolezo juu ya kubomolewa hekalu
(Utenzi wa Asafu)
1Kwa nini, ee Mungu, umetutupa kabisa?
Mbona hasira yako inawaka dhidi ya kondoo wako!
2Kumbuka jumuiya yako uliyojipatia tangu kale,
kabila ulilolikomboa liwe mali yako,
kumbuka mlima Siyoni mahali unapokaa.
3Pita juu ya magofu haya ya kudumu!
Adui wameharibu kila kitu hekaluni.
4Maadui zako wamenguruma ushindi hekaluni mwako!
Wameweka humo bendera zao za ushindi!
5Wanafanana na mtema kuni,
anayekata miti kwa shoka lake.#74:5 aya hii katika Kiebrania si dhahiri.
6Waliivunjavunja milango ya hekalu,
kwa mashoka na nyundo zao.
7Walichoma moto patakatifu pako;
walikufuru mahali pale unapoheshimiwa.
8Walipania kutuangamiza sote pamoja;
walichoma kila mahali tulipokutania kukuabudu nchini.
9Hatuzioni tena ishara zetu takatifu,
hatuna tena nabii yeyote!
Hata hatujui yatakuwa hivi hadi lini!
10Mpaka lini, ee Mungu, adui atakucheka?
Je, watalikufuru jina lako milele?
11Mbona umeuficha mkono wako?
Kwa nini hunyoshi mkono wako?
12Hata hivyo wewe Mungu ni mfalme wetu tangu kale;
umefanya makuu ya wokovu katika nchi.
13Kwa enzi yako kuu uliigawa bahari;
uliviponda vichwa vya majoka ya bahari.
14 # Taz Zab 104:26 Wewe uliviponda vichwa vya dude Lewiyathani;
ukawapa wanyama wa jangwani mzoga wake.
15Wewe umefanya chemchemi na vijito;
na kuikausha mito mikubwa.
16Mchana ni wako na usiku ni wako;
umeweka mwezi na jua mahali pao.
17Wewe umeweka mipaka yote ya dunia;
umepanga majira ya kiangazi na ya baridi.
18Kumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, madharau ya maadui zako;
taifa pumbavu linalikashifu jina lako.
Sisi ni dhaifu kama njiwa.
19Usiwatupie wanyama wakali uhai wa wapenzi wako;
usiyasahau maisha ya maskini wako.#74:19 Kiebrania: Roho ya njiwa wako; lakini yawezekana kwamba mwandishi alikuwa anafananisha udhaifu wa watu na njiwa! Kwa maana hiyo roho ya njiwa wako na maisha ya maskini wako ni sambamba.
20Ulikumbuke agano ulilofanya nasi!
Nchi imejaa uharamia kila mahali pa giza.
21Usiwaache wanaokandamizwa waaibishwe,
uwajalie maskini na wahitaji walisifu jina lako.
22Inuka, ee Mungu, ukajitetee;
ukumbuke wanavyokudharau kila siku watu wasiokujua.
23Usisahau makelele za maadui zako;
na ghasia za daima za wapinzani wako.

Currently Selected:

Zaburi 74: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy