YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 45

45
Utenzi wa kumsifu mfalme#45 Zaburi ya kifalme: Lakini tofauti na iliyotangulia kwa kuwa huu sio utenzi unaoelekezwa kwa Mungu ila ni utenzi kwa sifa ya mfalme. Wakristo wa kwanza walifafanua Zaburi hii wakifikiria Masiha. Taz Ebr 1:8-9.
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yungiyungi. Utenzi wa Wakorahi; utenzi wa mapenzi)
1Moyo wangu umejaa mawazo mema:
Namtungia mfalme shairi langu,
ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
2Wewe u mzuri kuliko wanadamu wote,
maneno yako ni fadhili tupu.
Kwa hiyo Mungu amekubariki milele.
3Jifunge upanga wako, ewe shujaa!
Wewe ni mtukufu na mwenye fahari.
4Songa mbele kwa utukufu upate ushindi,
utetee ukweli na kulinda haki.
Mkono wako utende mambo makuu.
5Mishale yako ni mikali,
hupenya mioyo ya maadui za mfalme;
nayo mataifa huanguka chini yako.
6 # Taz Ebr 1:8-9 Kiti chako cha enzi ni imara,#45:6 kiti … imara: Au Ee Mungu, kiti chako cha enzi chadumu milele na milele.
chadumu milele kama cha Mungu.
Wewe watawala watu wako kwa haki.
7Wapenda uadilifu na kuchukia uovu.
Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuteua,
na kukupa furaha kuliko wenzako.
8Mavazi yako yanukia marashi na udi,
wanamuziki wakuimbia katika majumba ya pembe za ndovu.
9Binti za wafalme ni baadhi ya wanaokulaki,
naye malkia amesimama kulia kwako,
amevaa mapambo ya dhahabu safi ya Ofiri.
10Sikiliza binti, ufikirie!
Tega sikio lako:
Sahau sasa watu wako na jamaa zako.
11Uzuri wako wamvutia mfalme;
yeye ni bwana wako, lazima umtii.
12Watu wa Tiro watakuletea zawadi;
matajiri watataka upendeleo wako.
13Binti mfalme anaingia mzuri kabisa!
Vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.
14Akiwa amevalia vazi la rangi nyingi,
anaongozwa kwa mfalme,
akisindikizwa na wasichana wenzake;
nao pia wanapelekwa kwa mfalme.
15Kwa furaha na shangwe wanafika huko,
na kuingia katika jumba la mfalme.
16Ee mfalme, utapata watoto wengi
watakaotawala mahali pa wazee wako;
utawafanya watawale duniani kote.
17Nitalifanya jina lako litukuzwe katika vizazi vyote,
nayo mataifa yatakusifu daima na milele.

Currently Selected:

Zaburi 45: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy