YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 17

17
Sala ya mtu mwema
(Sala ya Daudi)
1Ee Mwenyezi-Mungu usikie kisa changu cha haki,
usikilize kilio changu,
uitegee sikio sala yangu isiyo na hila.
2Haki yangu na ije kutoka kwako,
kwani wewe wajua jambo lililo la haki.
3Wewe wajua kabisa moyo wangu;
umenijia usiku, kunichunguza,
umenitia katika jaribio;
hukuona uovu ndani yangu,
sikutamka kitu kisichofaa.
4Kuhusu matendo watendayo watu;
mimi nimeitii amri yako,
nimeepa njia ya wadhalimu.
5Nimefuata daima njia yako;
wala sijateleza kamwe.
6Nakuita, ee Mungu, kwani wewe wanijibu;
unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.
7Onesha fadhili zako za ajabu,
uwaokoe kutoka kwa adui zao,
wale wanaokimbilia usalama kwako.
8Unilinde kama mboni ya jicho;
unifiche kivulini mwa mabawa yako,
9mbali na mashambulio ya waovu,
mbali na maadui zangu hatari wanaonizunguka.
10Hao hawana huruma yoyote moyoni;
wamejaa maneno ya kujigamba.
11Wananifuatia na kunizunguka;
wananivizia waniangushe chini.
12Wako tayari kunirarua kama simba:
Kama mwanasimba aviziavyo mawindo.
13Inuka, ee Mwenyezi-Mungu,
uwakabili na kuwaporomosha.
Kwa upanga uiokoe nafsi yangu kutoka kwa waovu.
14Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu,
uniokoe mikononi mwa watu hao,
watu ambao riziki yao ni dunia hii tu. #17:14 makala ya Kiebrania si dhahiri.
Uwajaze adhabu uliyowawekea,
wapate ya kuwatosha na watoto wao,
wawaachie hata na wajukuu zao.
15Lakini mimi nitauona uso wako, kwani ni mwadilifu;
niamkapo nitajaa furaha kwa kukuona.

Currently Selected:

Zaburi 17: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy