YouVersion Logo
Search Icon

Wafilipi UTANGULIZI

UTANGULIZI
Barua kwa jumuiya ya Wakristo kule Filipi iliandikwa wakati Paulo alipokuwa kifungoni labda kati ya mwaka 55 mpaka 63 B.K. Mji wa Filipi ulikuwa magharibi ya Makedonia katika nchi ambayo sasa ni Ugiriki, upande wa kaskazini. Wafilipi wanatajwa kwa mara ya kwanza katika Agano Jipya katika Mate 16:12 Huo ulikuwa mji wa kwanza huko Ulaya ambamo Paulo alihubiri Habari Njema akitokea Troa, wakati wa ziara yake ya pili ya kitume.
Jumuiya ya Wakristo huko Filipi ndiyo peke yake iliyompenda Paulo na kumsaidia katika shughuli zake alipokuwa anaondoka Makedonia na baadaye wakati akiwa kifungoni (taz 2Kor 11:8-9). Paulo anawaandikia Wakristo wa Filipi kuwashukuru kwa zawadi zao ambazo Epafrodito alimletea; anawapa mawaidha mbalimbali na kuwatia moyo wazingatie mfano wa Kristo. Paulo anawatahadharisha wasomaji wake pia juu ya vikundi vilivyozingatia mafundisho ya Wayahudi na ambavyo vilisababisha fujo kati ya waumini.
Barua hii yajulikana kuwa “barua ya furaha” maana jambo la furaha linagusiwa katika barua hii mara kwa mara. Furaha hiyo ina msingi wake katika kuwa na uaminifu kwa Kristo ambaye kazi yake yaelezwa kwa lugha maalumu ya utenzi (2:6-11). Barua yenyewe haioneshi kuwa na muundo ulio wazi wa mafundisho. Lakini inaonekana kuwa na mawazo yenye nguvu ya pekee pamoja na mashauri ya kufaa kwa maisha ya Wakristo na mwendo wa kanisa kwa jumla.
Baada ya maneno ya mwanzo ya shukrani na sala kwa ajili ya Wafilipi (1:3-11), mawazo mawili yanachukua nafasi kubwa katika hii barua: Furaha ambayo inatokana na imani iliyokomaa, na mapendo ya Paulo kwa kanisa la Filipi.
Sehemu kubwa ya barua hii (1:12–4:20) imetanguliwa na maneno ya kuanzia (1:1-11) yenye maneno ya shukrani na sala ambavyo vinaonesha jinsi Paulo alivyopendezwa na maisha ya Wafilipi, na mwisho wa sehemu hiyo kubwa yanafuata maneno ya kumalizia (4:21-23) ambayo yanadhihirisha ukarimu wa Wakristo wa Filipi.

Currently Selected:

Wafilipi UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy