YouVersion Logo
Search Icon

Yoeli UTANGULIZI

UTANGULIZI
Hatujui mengi kumhusu huyu nabii Yoeli licha ya yale tunayoambiwa kwa ufupi sana mwanzoni mwa kitabu hiki, wala hatuwezi kusema kwa uhakika aliishi nyakati zipi. Yakisiwa kwamba maandishi hayo ni ya kati ya miaka 800 – 300 K.K. Baadhi ya mambo yanayosemwa na namna yanavyosemwa yaonesha kwamba maandishi hayo ni ya namna ile ya maandiko ya ufasaha wa “Mambo ya mwisho” (Apokaliptiki) ambayo yapatikana pia katika kitabu cha Isaya, Zekaria na Danieli na katika kitabu cha Ufunuo. Tazama pia utangulizi wa vitabu hivyo.
Kitabu hiki kinataja tukio la kutisha la nzige ambalo lilizuka pamoja na ukame nchini kote. Katika tukio hilo mwandishi anaona na kutangaza kuja kwa “Siku ya Mwenyezi-Mungu.” Kwake ni dhahiri kwamba Mungu atachukua hatua ya kuwaadhibu wote wanaopinga matakwa yake.
Yoeli anawataka viongozi wa watu wafanye mfungo ili wapate kumrudia Mungu kikamilifu. Anawakumbusha watu yale aliyoahidi Mungu kuwa watakombolewa. Ahadi mojawapo ya Mungu ni kwamba atawamiminia watu wote roho yake, wanaume na wanawake, watoto na wazee (2:28-32). Katika Agano Jipya ahadi hiyo ya Mungu imechukuliwa kukamilika kwa kuja kwake Roho Mtakatifu (taz Matendo 2:17-21).

Currently Selected:

Yoeli UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy