YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 11

11
Ufalme wa amani
1 #11:1 Taz Ufu 5:5; 22:16 Kutatokea chipukizi katika kisiki cha Yese,
tawi litachipua mizizini mwake.
2Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,
roho ya hekima na maarifa,
roho ya shauri jema na nguvu,
roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.
3Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.
Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,
wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.
4 #11:4 Taz 2Thes 2:8 Atawapatia haki watu maskini,
atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.
Kwa neno lake ataiadhibu dunia,
kwa tamko lake atawaua waovu.
5 #11:5 Taz Efe 6:14 Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,
uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.
6 #11:6-9 Taz Isa 65:25 Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,
chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.
Ndama na wanasimba watakula pamoja,
na mtoto mdogo atawaongoza.
7Ngombe na dubu watakula pamoja,
ndama wao watapumzika pamoja;
na simba atakula majani kama ng'ombe.
8Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyoka
mtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.
9 #11:9 Taz Hab 2:14 Katika mlima mtakatifu wa Mungu
hakutakuwa na madhara wala uharibifu.
Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini,
kama vile maji yajaavyo baharini.
Walio uhamishoni watarudi
10 #11:10 Taz Roma 15:12 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka. 11Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani.
12Naye atatweka bendera kuwaashiria mataifa,
kuwakusanya Waisraeli waliodharauliwa,
kuwaleta pamoja watu wa Yuda waliotawanywa,
na kuwarudisha toka pembe nne za dunia.
13Wivu wa Efraimu juu ya Yuda utakoma,
hakutakuwa tena na uadui kati ya Yuda na Efraimu.
14Wote pamoja watawavamia Wafilisti walio magharibi,
pamoja watawapora watu wakaao mashariki.
Watawashinda Waedomu na Wamoabu,
nao Waamoni watawatii.
15Mwenyezi-Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Shamu,#11:15 bahari ya Shamu: Kiebrania: Bahari ya Misri.
kwa pumzi yake ichomayo atakausha mto Eufrate,
nao utagawanyika katika vijito saba,
watu wavuke humo miguu mikavu.
16Tena, kutakuwa na barabara kuu toka Ashuru
kwa ajili ya watu wake waliobaki humo
kama ilivyokuwa kwa Waisraeli
wakati walipotoka nchini Misri.

Currently Selected:

Isaya 11: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy