YouVersion Logo
Search Icon

Zab 91

91
Hakikisho la Ulinzi wa Mungu
1Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
3Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,
Na katika tauni iharibuyo.
4 # Zab 61:4 Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 # Ayu 5:19; Mit 3:23; Isa 43:2 Hutaogopa hofu ya usiku,
Wala mshale urukao mchana,
6Wala tauni ipitayo gizani,
Wala uele uharibuo adhuhuri,
7Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako.
Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume!
Hata hivyo hautakukaribia wewe.
8 # Mal 1:5 Ila kwa macho yako utatazama,
Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;
Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
10 # Mit 1:33; 2 The 3:3; 2 Pet 2:9 Mabaya hayatakupata wewe,
Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 # Mt 4:6; Lk 4:10 # Zab 34:7; Mt 4:6; Lk 4:10; Ebr 1:14 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake
Wakulinde katika njia zako zote.
12 # Ayu 5:23; Zab 37:24; Mt 4:6; Lk 4:11 Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 # Lk 10:19 Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
14Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,
Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 # Ayu 22:27; Zab 18:3; Yer 33:3; Zek 13:9; Ebr 5:7; Zab 43:2; 1 Sam 2:30 Ataniita nami nitamwitikia;
Nitakuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza;
16Kwa siku nyingi nitamshibisha,
Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

Currently Selected:

Zab 91: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy