YouVersion Logo
Search Icon

Mk 9

9
Kugeuka Sura
1Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.
2 # 2 Pet 1:17-18 Hata baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao; 3mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe. 4Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu. 5Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. 6Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi. 7#Mt 3:17; Mk 1:11; Lk 3:22; 2 Pet 1:17; Kum 18:15; Mdo 3:22Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. 8Mara hiyo walipotazama huku na huku, hawakuona mtu pamoja nao ila Yesu peke yake.
Kuja kwa Eliya
9 # Mk 8:30 Na walipokuwa wakishuka mlimani aliwakataza wasimweleze mtu waliyoyaona, hata Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu. 10Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huko kufufuka katika wafu maana yake nini? 11#Mal 4:5; Mt 11:14Wakamwuliza, wakisema, Mbona waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 12#Mal 4:5; Isa 53:3Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza upya yote; lakini, pamoja na haya, ameandikiwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharauliwa? 13#Mt 11:14; 1 Fal 19:2,10Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa.
Kuponya kwa Mvulana mwenye Pepo
14 # Mt 17:14-21; Lk 9:37-42 Hata walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao; 15mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. 16Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? 17Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; 18na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. 19Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu. 20Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. 21Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. 22Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. 23#Mk 11:23Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24#Lk 17:5Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. 25Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. 26#Mk 1:26Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. 27Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama. 28Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 29Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.
Yesu Asema juu ya Kufa na Kufufuka kwake tena
30 # Mt 17:22,23; Lk 9:43-45 # Yn 7:1 Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua. 31#Mk 8:31; 10:32-34Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. 32#Lk 9:45; 18:34Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza.
Ni nani Mkubwa wa Wote
33 # Mt 18:1-9; Lk 9:46-50 # Mt 17:24 Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? 34#Lk 22:24Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. 35#Mt 20:26-27; 23:11; Mk 10:43-44; Lk 22:26Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote. 36#Mk 10:16Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, 37#Mt 10:40; Lk 10:16; Yn 13:20Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Mtoa Pepo Mwingine
38 # Hes 11:27,28 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. 39#1 Kor 12:3Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya; 40#Mt 12:30; Lk 11:23kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu. 41#Mt 10:42Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
Majaribu ya Dhambi
42Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. 43#Mt 5:30Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; [ 44ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 45Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [ 46ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 47#Mt 5:29Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; 48#Isa 66:24ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 49#Law 2:13Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto. 50#Mt 5:13; Lk 14:34-35; Kol 4:6Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.

Currently Selected:

Mk 9: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy