YouVersion Logo
Search Icon

Ayu 42

42
Ayubu Anyenyekezwa na Kutoshelezwa
1Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema.
2 # Yer 32:17; Mt 3:9; Mk 14:36; Lk 1:37; Efe 3:20 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote,
Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.
3 # Ayu 38:2; 1 Tim 1:7; Zab 40:5 Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa?
Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu,
Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.
4 # Ayu 38:3 Sikiliza, nakusihi, nami nitanena;
Nitakuuliza neno, nawe niambie.
5 # Rum 10:17; Hes 12:8,9; Isa 6:1 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio;
Bali sasa jicho langu linakuona.
6Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu
Katika mavumbi na majivu.
Marafiki wa Ayubu Waaibishwa
7Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 8#Hes 23:1; Ebr 10:4; Mt 5:24; Mwa 20:17; Ebr 7:25; Yak 5:16Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 9Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile BWANA alivyowaamuru; naye BWANA akamridhia Ayubu.
Ayubu Arejeshewa Mali yake Maradufu
10 # Ayu 1:1-3; Isa 40:2 Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza. 11#Ayu 19:13Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote BWANA aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. 12#Ayu 8:7; 1:3Basi hivyo BWANA akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu. 13Tena alikuwa na wana waume saba, na binti watatu. 14Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. 15Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. 16#Ayu 5:26Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne. 17#Mwa 25:8Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku.

Currently Selected:

Ayu 42: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy