YouVersion Logo
Search Icon

Mwa 18

18
Abrahamu na Sara Waahidiwa Mtoto
1 # Mwa 13:18; 14:13; Mdo 7:2 BWANA akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. 2#Ebr 13:2; Mwa 18:22; 19:1; 1 Pet 4:9Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, 3akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. 4#Mwa 24:32; 43:24Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. 5Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.
6Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. 7Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng’ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. 8Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
9 # Mwa 24:67; Tit 2:5 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. 10#Rum 9:9; Mwa 21:2; Lk 1:13Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. 11#Rum 4:19; Ebr 11:11Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12#1 Pet 3:6; Lk 1:18; Mwa 17:17Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? 13BWANA akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? 14#Lk 1:37; Zab 115:3; Yer 32:17; Zek 8:6; Mt 3:9; 19:26; Rum 4:21; Ebr 11:19Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. 15Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.
Abrahamu Aiombea Sodoma
16Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize. 17#Zab 25:14; Amo 3:7; Yn 15:15BWANA akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, 18#Mwa 12:3; 22:18; Zab 72:17; Mdo 3:25; Gal 3:8,9,16,18akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? 19#Kum 6:6,7; Yos 24:15; Efe 6:4Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. 20#Mwa 4:10; 19:13; Yak 5:4BWANA akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, 21#Mwa 11:5; Kut 3:8; Zab 14:2; Ebr 4:13basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua. 22#Mwa 18:1,2Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za BWANA.
23 # Hes 16:22; 2 Sam 24:17; Zab 11:4-7 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? 24#Mt 7:13,14Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? 25#Isa 3:10,11; Ayu 8:3,20; Zab 58:11; 94:2; Rum 3:5,6Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? 26#Yer 5:1; Eze 22:30; Mt 24:22BWANA akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
27 # Lk 18:1; Zab 8:4 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. 28Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. 29#1 The 5:17Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.
30 # Isa 55:8,9 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. 31#Ebr 4:16Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. 32#Amu 6:39; Kut 34:6,7; Zab 34:15; Mit 15:29; 1 Yoh 3:22; Yak 5:16Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. 33Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.

Currently Selected:

Mwa 18: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy