YouVersion Logo
Search Icon

Gal 6

6
Chukulianeni Mizigo
1 # Mt 18:15; Yak 5:19 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. 2Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. 3Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. 4#2 Kor 13:5Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. 5#Rum 14:12Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.
6 # 1 Kor 9:14 Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote. 7Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. 8#Rum 8:13; Yn 6:63; 3:6Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 9#2 The 3:13Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. 10#2 Pet 1:7Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Mawaidha ya Mwisho na Baraka
11Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe! 12#Gal 5:11; Flp 3:18Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu. 13Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. 14#1 Kor 1:31; 2:2Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. 15#Gal 5:6; 1 Kor 7:19Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. 16#Zab 125:5; 128:6; Flp 3:3Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.
17 # 2 Kor 4:10 Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.
18Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina.

Currently Selected:

Gal 6: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy