YouVersion Logo
Search Icon

1 Yoh 3

3
1 # Yn 1:12,13; 16:3; 1 Yoh 5:20 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2#1 Yoh 2:28; Rum 8:17; 2 Kor 3:18; Flp 3:21; Kol 3:4; Kut 34:29Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. 4#Mt 7:23Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 5#Yn 1:29; Isa 53:4; 1 Pet 2:24Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 6#Rum 6:14Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 7#1 Yoh 2:29Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; 8#Yn 8:44atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 9#1 Yoh 5:18Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 10Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Pendaneni Ninyi kwa Ninyi
11 # Yn 13:34; 15:12 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi; 12#Mwa 4:8si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
13 # Mt 5:11; Yn 15:18,19 Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia. 14#Yn 5:24; 1 Yoh 2:11Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. 15#Mt 5:21,22; Yn 8:44Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. 16#Yn 13:1; 15:13; Gal 2:20Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. 17#1 Yoh 4:20; Kum 15:7Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18#Yak 1:22; 2:15,16Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. 19Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, 20ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote. 21#Rum 5:1; Ebr 4:16Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; 22#Mk 11:24na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. 23#Yn 6:29; 13:34; 15:12,17Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. 24#1 Yoh 4:13; Rum 8:9Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.

Currently Selected:

1 Yoh 3: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy