Ufunuo 19:7-8
Ufunuo 19:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa harusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari. Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu).
Ufunuo 19:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye ameruhusiwa kuvikwa kitani nzuri, ing'aayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
Ufunuo 19:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.