Ufunuo 19:3-4
Ufunuo 19:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakasema, “Asifiwe Mungu! Moshi wa moto unaoteketeza mji huo utapanda juu milele na milele!” Na wale wazee ishirini na wanne, na wale viumbe hai wanne, wakajitupa chini, wakamwabudu Mungu aliyeketi juu ya kiti cha enzi wakisema, “Amina! Asifiwe Mungu!”
Ufunuo 19:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.
Ufunuo 19:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.
Ufunuo 19:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakasema tena kwa nguvu: “Haleluya! Moshi wake huyo kahaba unapanda juu milele na milele.” Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wanne wenye uhai wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, aliyekuwa ameketi kwenye kile kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu: “Amen, Haleluya!”