Zaburi 77:12-14
Zaburi 77:12-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitatafakari juu ya kazi zako, na kuwaza juu ya matendo yako makuu. Kila ufanyacho ee Mungu, ni kitakatifu. Ni mungu gani aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ni Mungu unayetenda maajabu; wewe umeyaonesha mataifa uwezo wako.
Zaburi 77:12-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. Ee Mungu, njia yako iko katika utakatifu; Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.
Zaburi 77:12-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.