Zaburi 30:1-3
Zaburi 30:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, nakutukuza maana umeniokoa, wala hukuwaacha maadui zangu wanisimange. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, nilikulilia msaada, nawe ukaniponya. Ee Mwenyezi-Mungu, umeniokoa kutoka kuzimu; umenipa tena uhai, umenitoa miongoni mwa waendao kuzimu.
Zaburi 30:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu. Ee BWANA, Mungu wangu, Nilikulilia ukaniponya. Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.
Zaburi 30:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu. Ee BWANA, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya. Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.
Zaburi 30:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nitakutukuza wewe, Ee BWANA, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu. Ee BWANA, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. Ee BWANA, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.