Zaburi 119:5-8
Zaburi 119:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Laiti mwenendo wangu ungeimarika, kwa kuyafuata masharti yako! Nikizingatia amri zako zote, hapo kweli sitaaibishwa. Nitakusifu kwa moyo mnyofu, nikijifunza maagizo yako maadilifu. Nitayafuata masharti yako; usiniache hata kidogo.
Zaburi 119:5-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako. Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa.
Zaburi 119:5-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa