Zaburi 119:35-37
Zaburi 119:35-37 Biblia Habari Njema (BHN)
Uniongoze katika njia ya amri zako, maana humo napata furaha yangu. Unipe ari ya kuzingatia maamuzi yako, na si kwa ajili ya kupata faida isiyofaa. Uniepushe, nisifuate mambo ya upuuzi; unioneshe njia yako, unipe uhai.
Zaburi 119:35-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Uniendeshe katika mapito ya amri zako, Kwa maana nimependezwa nayo. Unielekeze moyo wangu katika shuhuda zako, Wala usiielekee tamaa. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.
Zaburi 119:35-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, Kwa maana nimependezwa nayo. Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako, Wala usiielekee tamaa. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.
Zaburi 119:35-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha. Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi. Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.