Zaburi 119:150-152
Zaburi 119:150-152 Biblia Habari Njema (BHN)
Wale wanaonidhulumu vibaya wanakaribia, hao wako mbali kabisa na sheria yako. Lakini wewe u karibu nami, ee Mwenyezi-Mungu, na amri zako zote ni za kuaminika. Tangu zamani, nimejifunza maamuzi yako; ambayo umeyaweka hata yadumu milele.
Zaburi 119:150-152 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki, Wamekwenda mbali na sheria yako. Ee BWANA, Wewe U karibu, Na maagizo yako yote ni kweli. Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako, Ya kuwa umeziweka zikae milele.
Zaburi 119:150-152 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki, Wamekwenda mbali na sheria yako. Ee BWANA, Wewe U karibu, Na maagizo yako yote ni kweli. Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako, Ya kuwa umeziweka zikae milele.
Zaburi 119:150-152 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, lakini wako mbali na sheria yako. Ee BWANA, hata hivyo wewe u karibu, na amri zako zote ni za kweli. Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.