Zaburi 119:126-128
Zaburi 119:126-128 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, sasa ni wakati wa kufanya kitu, kwa maana watu wanavunja sheria yako. Mimi, nazipenda amri zako, kuliko hata dhahabu safi kabisa. Kwa hiyo, nafuata kanuni zako zote; kila njia potovu naichukia.
Zaburi 119:126-128 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakati umewadia BWANA atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako. Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi. Maana nayafuata mausia yako yote, kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia.
Zaburi 119:126-128 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakati umewadia BWANA atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako. Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi. Maana nayaona mausia yako yote kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia.