Methali 31:1-3
Methali 31:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake: Nikuambie nini mwanangu? Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa? Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu? Usimalize nguvu zako kwa wanawake, usiwape mali yako hao wanaoangamiza wafalme.
Methali 31:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake. Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wanaowaharibu wafalme.
Methali 31:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake. Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.