Methali 24:23-25
Methali 24:23-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima: Kupendelea watu katika hukumu si vizuri. Anayemwachilia mtu mwenye hatia, hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa. Lakini wanaowaadhibu waovu watapata furaha, na baraka njema zitawajia.
Methali 24:23-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Makabila ya watu watamlaani, taifa watamchukia. Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.
Methali 24:23-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia. Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.
Methali 24:23-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema: Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” Kabila zitamlaani na mataifa yatamkana. Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, nazo baraka tele zitawajilia juu yao.