Filemoni 1:21-25
Filemoni 1:21-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba. Pamoja na hayo, nitayarishie chumba kwani natumaini kwamba kwa sala zenu, Mungu atanijalia niwatembeleeni. Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu, anakusalimu. Nao akina Marko, Aristarko, Dema na Luka, wafanyakazi wenzangu, wanakusalimu. Nawatakieni nyinyi nyote neema ya Bwana Yesu Kristo.
Filemoni 1:21-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana natumaini ya kwamba kwa maombi yenu nitarejeshwa kwenu. Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu; na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.
Filemoni 1:21-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana nataraji ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata. Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu; na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.
Filemoni 1:21-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba. Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu. Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu, anakusalimu. Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.