Mika 6:3-5
Mika 6:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Enyi watu wangu, nimewatendea nini? Nimewachosha kwa kitu gani? Nijibuni! Mimi niliwatoa nchini Misri; niliwakomboa kutoka utumwani; niliwapeni Mose, Aroni na Miriamu kuwaongoza. Enyi watu wangu, kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu, na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu. Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali. Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”
Mika 6:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Enyi watu wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa kitu gani? Shuhudieni juu yangu. Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako. Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni yaliyotukia toka Shitimu hadi Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.
Mika 6:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Enyi watu wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa habari gani? Shuhudieni juu yangu. Kwa maana nalikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami naliwapeleka Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako. Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni toka Shitimu hata Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.
Mika 6:3-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Watu wangu, nimewatendea nini? Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu. Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa. Nilimtuma Mose awaongoze, pia Aroni na Miriamu. Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu alivyofanya shauri na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu. Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali, ili mfahamu matendo ya haki ya BWANA.”