Mathayo 12:15-17
Mathayo 12:15-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata, akawaponya wagonjwa wote, akawaamuru wasiwaambie watu habari zake, ili yale aliyosema Mungu kwa njia ya nabii Isaya yatimie
Mathayo 12:15-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote, akawakataza wasimdhihirishe; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema
Mathayo 12:15-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote, akawakataza wasimdhihirishe; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema
Mathayo 12:15-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Yesu alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote, akiwakataza wasiseme yeye ni nani. Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema