Luka 8:22-23
Luka 8:22-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ngambo.” Basi, wakaanza safari. Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya mashua, wakawa katika hatari.
Luka 8:22-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa siku zile mojawapo alipanda katika mashua yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, mashua ikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
Luka 8:22-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
Luka 8:22-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Siku moja Yesu alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni twende mpaka ngʼambo ya ziwa.” Nao wakaondoka. Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.