Luka 8:19-21
Luka 8:19-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo mama na ndugu zake Yesu wakamjia, lakini hawakuweza kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu. Yesu akapewa habari kwamba mama na ndugu zake walikuwa nje, wanataka kumwona. Lakini Yesu akawaambia watu wote, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika.”
Luka 8:19-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo mama yake na ndugu zake wakamwendea, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano. Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe. Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ni hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.
Luka 8:19-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano. Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe. Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.
Luka 8:19-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati mmoja mama yake Yesu na ndugu zake walikuja kumwona, lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.” Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulifanya.”