Luka 2:50-52
Luka 2:50-52 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu.
Luka 2:50-52 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nao hawakuelewa neno hilo alilowaambia. Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake. Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Luka 2:50-52 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake. Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Luka 2:50-52 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini wao hawakuelewa maana ya lile alilowaambia. Ndipo akashuka pamoja nao hadi Nazareti, naye alikuwa mtiifu kwao. Lakini mama yake akayaweka moyoni mwake mambo haya yote. Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.