Luka 12:57-59
Luka 12:57-59 Biblia Habari Njema (BHN)
“Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya? Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani. Hakika hutatoka huko, nakuambia, mpaka utakapomaliza kulipa senti ya mwisho.”
Luka 12:57-59 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya hakimu; yule hakimu akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi umalize kulipa hata senti ya mwisho.
Luka 12:57-59 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Luka 12:57-59 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kwa nini hamwamui wenyewe lililo haki? Uwapo njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani. Nakuambia, hautatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho.”