Walawi 7:25-27
Walawi 7:25-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtu yeyote akila mafuta ya mnyama aliyetolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atatengwa na watu wake. Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi. Mtu yeyote akila damu yoyote, atatengwa na watu wake.”
Walawi 7:25-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa BWANA kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake. Tena msiile damu yoyote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. Mtu yeyote alaye damu, mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.
Walawi 7:25-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa BWANA kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake. Tena msiile damu yo yote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. Mtu ye yote alaye damu, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
Walawi 7:25-27 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mtu yeyote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwa BWANA kwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. Popote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege yeyote wala ya mnyama. Ikiwa mtu yeyote atakunywa damu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”