Walawi 7:22-24
Walawi 7:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie Waisraeli hivi: Msile mafuta ya ng'ombe au ya kondoo au ya mbuzi. Mafuta ya mnyama yoyote aliyekufa mwenyewe au ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini yaweza kuwekwa kwa matumizi mengine, lakini kamwe msiyale.
Walawi 7:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yoyote, ya ng'ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi. Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa matumizi mengine; lakini msiyale kamwe.
Walawi 7:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yo yote, ya ng’ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi. Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa ajili ya matumizi mengine; lakini msiyale kabisa.