Walawi 7:16-17
Walawi 7:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini kama sadaka hiyo ya amani ni ya nadhiri au ya hiari, italiwa siku hiyohiyo inapotolewa na sehemu nyingine yaweza kuliwa kesho yake. Lakini nyama yoyote ya sadaka hiyo inayobaki hadi siku ya tatu itateketezwa.
Walawi 7:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini ikiwa hii sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia kitaliwa; lakini hicho kitakachosalia, katika hizo nyama za sadaka, hata siku ya tatu kitachomwa moto.
Walawi 7:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini kwamba hii sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia kitaliwa; lakini hicho kitakachosalia, katika hizo nyama za sadaka, hata siku ya tatu kitachomwa moto.
Walawi 7:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“ ‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini chochote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake. Nyama yoyote ya sadaka inayobaki mpaka siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto.