Walawi 19:7-8
Walawi 19:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama sehemu ya nyama yake italiwa siku ya tatu, tendo hilo ni chukizo; na sadaka hiyo haitakubaliwa, naye atakayekula nyama hiyo ni lazima awajibike kwa uovu wake kwa sababu amekitia unajisi kitu kitakatifu cha Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo atatengwa na watu wake.
Walawi 19:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikiwa sadaka hiyo inaliwa hata kidogo siku ya tatu ni machukizo; haitakubaliwa; lakini kila mtu atakayekula atalipizwa uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha BWANA; na mtu huyo atatengwa na watu wake.
Walawi 19:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwamba sadaka hiyo yaliwa hata kidogo siku ya tatu ni machukizo; haitakubaliwa; lakini kila mtu atakayekula atauchukua uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha BWANA; na nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.