Yona 4:9-11
Yona 4:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Mungu akamwambia Yona, “Je, unadhani wafanya vema kuukasirikia mmea huo?” Yona akajibu, “Ndiyo, nafanya vema kukasirika – kukasirika hata kufa!” Hapo Mungu akamwambia, “Mmea huu uliota na kukua kwa usiku mmoja, na usiku uliofuata ukanyauka. Wewe hukuufanyia kitu chochote, wala hukuuotesha. Mbona unauhurumia? Je, haifai kwangu kuuhurumia mji wa Ninewi, ule mji mkuu wenye watu 120,000, wasioweza kupambanua jema na baya, na pia wanyama wengi?”
Yona 4:9-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa. Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya elfu mia moja na ishirini, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Yona 4:9-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa. Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Yona 4:9-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?” Akasema, “Ndiyo, ninayo haki. Nimekasirika kiasi cha kufa.” Lakini BWANA akamwambia, “Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja. Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ngʼombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”