Yona 4:1-3
Yona 4:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini jambo hilo halikumpendeza Yona hata kidogo, akakasirika sana. Kwa hiyo akaomba, “Mwenyezi-Mungu, je, hayo si mambo yaleyale niliyowaza utayafanya nilipokuwa nyumbani? Ndio maana nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi. Nilijua kwamba wewe u Mungu wa upendo na huruma. Hukasiriki upesi, daima u mwema na u tayari kubadili nia yako wakati wowote ili usiadhibu. Basi, sasa ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi uniondolee uhai wangu, maana, kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kuishi.”
Yona 4:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika. Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nilijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya. Basi, sasa, Ee BWANA, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Yona 4:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika. Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya. Basi, sasa, Ee BWANA, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Yona 4:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. Akamwomba BWANA, “Ee BWANA, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa. Sasa, Ee BWANA, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”