Yobu 36:5-7
Yobu 36:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
“Sikiliza Mungu ni mwenye nguvu wala hamdharau mtu yeyote; uwezo wa akili yake ni mkuu mno! Hawaachi waovu waendelee kuishi; lakini huwapatia wanaodhulumiwa haki zao. Haachi kuwalinda watu waadilifu; huwatawaza, wakatawala na kutukuka.
Yobu 36:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu yeyote; Ana uweza katika nguvu za fahamu. Hauhifadhi uhai wa waovu; Lakini huwapa wateswao haki yao. Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.
Yobu 36:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote; Ana uweza katika nguvu za fahamu. Hauhifadhi uhai wa waovu; Lakini huwapa wateswao haki yao. Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.
Yobu 36:5-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake. Hawaachi waovu waendelee kuishi, bali huwapa walioteswa haki yao. Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme na kuwatukuza milele.