Yobu 36:20-23
Yobu 36:20-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Usitamani usiku uje, ambapo watu hufanywa watoweke walipo. Jihadhari! Usiuelekee uovu maana umepatiwa mateso kukuepusha na uovu. Kumbuka ukuu wa uwezo wa Mungu; nani awezaye kumfundisha kitu? Nani basi aliyeweza kumpangia njia yake, au awezaye kumwambia: ‘Umekosea?’
Yobu 36:20-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usiutamani usiku, Wakati watu wakatwapo katika mahali pao. Jitunze, usiutazame uovu; Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu. Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye? Ni nani aliyemwagiza njia yake? Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?
Yobu 36:20-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usiutamani usiku, Wakati watu wakatwapo katika mahali pao. Jitunze, usiutazame uovu; Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu. Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye? Ni nani aliyemwagiza njia yake? Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?
Yobu 36:20-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Usiutamani usiku uje, ili uwaburute watu mbali na nyumba zao. Jihadhari usigeukie uovu, ambao unaupenda zaidi kuliko mateso. “Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. Ni nani aliye mwalimu kama yeye? Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?