Yobu 36:1-4
Yobu 36:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Elihu akaendelea kusema: “Nivumilie kidogo, nami nitakuonesha kitu; maana bado ninacho cha kusema kwa niaba ya Mungu. Nitaleta hekima yangu kutoka mbali sana, na kuonesha kwamba Muumba wangu ni mwadilifu. Kweli maneno yangu si ya uongo; mwenye elimu kamili yuko hapa nawe.
Yobu 36:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena Elihu akaendelea na kusema, Ningojee kidogo nami nitakueleza; Kwa kuwa ningali na maneno kwa ajili ya Mungu. Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali, Nami nitampa haki Muumba wangu. Maana hakika maneno yangu si ya uongo; Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe.
Yobu 36:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena Elihu akaendelea na kusema, Ningojee kidogo nami nitakueleza; Kwa kuwa nikali na maneno kwa ajili ya Mungu. Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali, Nami nitampa haki Muumba wangu. Kwani yakini maneno yangu si ya uongo; Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe.
Yobu 36:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Elihu akaendelea kusema: “Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu. Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.