Yohane 12:41-43
Yohane 12:41-43 Biblia Habari Njema (BHN)
Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake. Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi. Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu.
Yohane 12:41-43 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake. Lakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi. Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.
Yohane 12:41-43 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake. Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi. Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.
Yohane 12:41-43 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake. Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.